Categories
sw-ke

Furaha

🤔 Furaha, furaha, afya: 1. Amani ya ndani. 2. Kupata kuridhika kutokana na kusaidia na kuwa tegemeo kwa Wengine. Mahusiano. 12R.tv❌✅ Nakutakia Wewe, Mimi na Wengine kwamba mwisho wa mwaka ujao, kila mmoja Wetu aseme: “2022 ulikuwa mwaka bora zaidi wa maisha yangu 🙂👍”. Marcin Ellwart

Furaha

Furaha ni mojawapo kati ya maono ya msingi, pamoja na pendo, hamu, chuki, hofu, huzuni na hasira. Furaha inapatikana pale ambapo umepata kile ulichokipenda na ulichokuwa na hamu nacho.

Neno hili tunaweza kutumia katika hali tofautitofauti. Wapo ambao watalitumia kama jina ila wengine ni hali ya kuwa na amani juu ya ufanyaji wa tendo fulani kwa kuwa hauwezi ukafanya kitu kwa furaha bila ya kuridhia mwenyewe au kuwa na amani nacho. Kwa kufanya hivyo unaweza ukafanya vibaya na kuharibu kabisa. Lakini kama umeridhia nacho, unaweza kufanya kitu hicho kwa umakini na kwa usahihi na unaweza kupendezwa nacho mwenyewe. Kwa mantiki hiyo basi tunaona kwamba katika maisha yetu ya kila siku si vyema kumlazimisha mtu mwingine afanye jambo ambalo hayuko tayari nalo kwa sababu anaweza akafanya kinyume kabisa na unavyotaka na kukusababishia matatizo mengine.

Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari.

Wikipedia.org:

https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Furaha

Kiswahili

Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (30%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.

Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.

Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu.

Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.

Kando ya Kiarabu toka zamani pia kuna athira ya lugha mbalimbali kama Kiajemi, Kihindi na Kireno.

Kuanzia karne ya 20 hadi sasa maneno mengi yamepokewa kutoka Kiingereza, na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kifaransa, lakini pia kutoka lugha nyingine, Kiarabu kikiwa mojawapo.

Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawahili au لغة سواحيلية lugha sawahiliya).

Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa.

Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika.

Tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea barani kwa njia ya biashara.

Wakati wa ukoloni wa Uingereza lugha ilisanifishwa na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye msingi wa lahaja ya Unguja.

https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Kiswahili

Kenya

Afrika Mashariki

Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi.

Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi).

Kenya ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.

Mji mkuu ni Nairobi.

Idadi ya watu imeongezeka sana katika miaka ya karibuni na kufikia milioni 49.

Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi aina elfu kadhaa za wanyama pori.

Jina la nchi limetokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika.

https://sw.m.wikipedia.org/wiki/Kenya

7hi7.com Sites.